Jumamosi 25 Aprili 2026 - 22:30
Israel chini ya shinikizo la kisiasa kutoka Ulaya

Hawza/ Maafisa wa utawala wa Israel wamekiri kuwa: wiki hii imekuwa wiki mbaya sana kwa Israel; Viktor Orbán, ambaye ametajwa kama mwenye mwelekeo wa kuisaidia Israel nchini Hungari, ameondolewa madarakani, na Italy imesimamisha mkataba muhimu wa ulinzi na Israel.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, mabadiliko haya yaliyotokea huenda yakasababisha Ulaya kupitia zaidi mikataba mingine iliyosimamishwa, ambayo ni matokeo ya vita na uvamizi wa utawala huu dhidi ya nchi mbalimbali pamoja na mauaji ya halaiki huko Ukanda Ghaza.

Maya Sion, mkurugenzi wa programu ya mahusiano ya Israel na Ulaya katika kituo cha tafiti cha Mitvim na pia mhadhiri katika Jukwaa la Ulaya la Chuo Kikuu cha Kiebrania cha Yerusalemu, alikiri kuwa; kura ya turufu ya Hungari ndiyo ilikuwa kizuizi pekee kilichokuwa kinazuia kupitishwa kwa kifurushi cha vikwazo dhidi ya walowezi wa Israel wenye misimamo ya vurugu barani Ulaya.

Ireland, Spain na Slovenia — ambazo ni miongoni mwa waungaji mkono wakuu wa suala la Palestina barani Ulaya — zimetaka kujadiliwa kwa wajibu wa haki za binadamu wa Israel kwa mujibu wa makubaliano yake ya ushirikiano na Umoja wa Ulaya, na ombi hili limetolewa wakati mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kukutana hivi karibuni.

Watu wengi barani Ulaya wanaotaka hatua kali zaidi dhidi ya Israel wanasema kuwa maadili ya msingi ya watu wa Ulaya yako hatarini, na kutokuchukua hatua kutasababisha kudhoofika kwa utawala wa sheria za kimataifa na utekelezwaji wa maadili hayo.

Chanzo: The Guardian

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha